Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo inatangaza nafasi 12 za Mtendaji wa Kijiji III. Fursa hii ni kwa wale wenye sifa zinazohitajika kujiunga na serikali katika ngazi ya kijiji.
Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji:
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao
- Kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo ya kijiji.
- Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za kijiji.
- Kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
- Kusimamia utungaji na utekelezaji wa sheria ndogo za kijiji.
Sifa zinazohitajika:
Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
Cheti cha Astashahada katika Utawala, Sheria, Maendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Fedha au fani nyingine zinazohusiana kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au chuo kinachotambulika na Serikali.
Faida:
Mshahara: TGS B
Mwisho wa Kutuma Maombi: 16 Oktoba 2024
Ikiwa una sifa, tafadhali tuma maombi yako kabla ya tarehe hiyo. Hii ni fursa nzuri ya kuchangia maendeleo ya kijiji na jamii kwa ujumla.
Post a Comment